Jeremiah 5:16-19


16 aPodo zao ni kama kaburi lililo wazi,
wote ni mashujaa hodari wa vita.

17 bWatayaangamiza mazao yenu na chakula chenu,
wataangamiza wana wenu na mabinti zenu;
wataangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ng’ombe,
wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu.
Kwa upanga wataangamiza
miji yenye maboma mliyoitumainia.

18“Hata hivyo katika siku hizo, sitakuangamiza kabisa,” asema Bwana. 19 c“Nao watu watakapouliza, ‘Kwa nini Bwana, Mungu wetu ametufanyia mambo haya yote?’ utawaambia, ‘Kama vile mlivyoniacha mimi na kutumikia miungu migeni katika nchi yenu wenyewe, ndivyo sasa mtakavyowatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.’
Copyright information for SwhKC